Google Ya Mafanikio
Ongea Na Kocha.
ONGEA NA KOCHA; Instant Cashflow Sehemu Ya Pili.
0:00
-3:06:08

ONGEA NA KOCHA; Instant Cashflow Sehemu Ya Pili.

Habari Mwanamafanikio?

Karibu kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA ambapo tunapata uchambuzi wa kitabu cha INSTANT CASHFLOW sehemu ya pili.

Kwenye sehemu hii ya pili tunaangalia maeneo mawili kati ya matano ya kukuza biashara.

Eneo la kwanza ni kutengeneza wateja tarajiwa kupitia masoko. Hapa tunaziangalia njia mbalimbali za masoko unazoweza kutumia kwenye biashara yako na ukawafikia wateja wengi wapya. Masoko ni sehemu muhimu sana ya biashara, isipofanyiwa kazi vizuri na kwa uhakika, biashara haiwezi kufanikiwa.

Eneo la tatu ni kuwageuza wateja tarajiwa kuwa wateja kamili. Unaweza kuwafikia wateja kwa njia za masoko, ila bado wasiwe tayari kununua. Unahitaji kuwa na njia za kuwashawishi wateja hao waweze kufanya manunuzi. Hapa unajifunza mbinu mbalimbali ambazo ukizitumia utaweza kuwashawishi wateja kununua.

Pamoja na hayo kuna michango mbalimbali kutoka kwa wanamafanikio wengine kuhusiana na yale ambayo tumejifunza.

Karibu sana usikilize kipindi hiki ambacho kina mengi ya kujifunza kwa ukuaji wa biashara yako.

Kocha.

0 Comments
Google Ya Mafanikio
Ongea Na Kocha.
Karibu kwenye vipindi vya sauti vya Ongea Na Kocha ambapo Kocha Dr Makirita Amani atakuwa anakushirikisha maarifa mbalimbali ya mafanikio pamoja na kujibu maswali na changamoto unazokutana nazo kwenye safari yako ya mafanikio.