May 16 • 2HR 52M

Ongea Na Kocha; Exactly What To Say, Mrejesho Wa Tathmini Ya Robo Mwaka Na Lengo Jipya La Namba Ya Mauzo.

 
1.0×
0:00
-2:51:31
Open in playerListen on);
Karibu kwenye vipindi vya sauti vya Ongea Na Kocha ambapo Kocha Dr Makirita Amani atakuwa anakushirikisha maarifa mbalimbali ya mafanikio pamoja na kujibu maswali na changamoto unazokutana nazo kwenye safari yako ya mafanikio.
Episode details
Comments

Habari mwanamafanikio?

Karibu kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA ambacho kina mambo matatu makubwa.

Jambo la kwanza ni mjadala wa kitabu cha EXACTLY WHAT TO SAY, kitabu chenye maneno 23 ya ushawishi ambayo ukiyatumia unakuwa na ushawishi mkubwa kwa wengine. Wanamafanikio wameshirikisha kwa mifano kuhusu maneno hayo. Sikiliza kipindi hiki kujifunza kutoka kwenye uzoefu wa wengine.

Jambo la pili ni mrejesho wa tathmini ya robo mwaka ya pili kwenye mwaka wetu wa mafanikio 2021/2022. Kwa ujumla bado watu wanapata changamoto kuripoti sehemu kubwa ya namba zinazopimwa kwenye tathmini. Tutaendelea kueleweshana hatua kwa hatua ili kuweza kuzielewa namba hizo kwa kina na kuweza kuzipima na kuziripoti. Kwenye kipindi hiki nimetoa tena ufafanuzi kuhusu namba muhimu tunazojitathmini nazo. Sikiliza kipindi ili uendelee kupata uelewa mkubwa wa namba hizo.

Jambo la tatu ni lengo jipya la namba ya mauzo ambalo nimempa kila mmoja. Baada ya kupitia tathmini za robo mwaka na kuona wengi tupo mbali sana na malengo tuliyonayo, nimechukua hatua ya kumpa kila mmoja lengo jipya la namba ya mauzo ambalo anapaswa kupambana kulifikia kila wiki. Ni namba kubwa kiasi ukilinganisha na mazoea ambayo mtu amekuwa anayapata na hivyo inamtaka mtu ajisukume kwa kila namna ili kufikia. Kwa kipindi kilichobakia kwenye mwaka wetu wa mafanikio, kila mmoja anapaswa kupambana na namba yake na kuweka mambo mengine yote pembeni.

Karibu usikilize kipindi hiki, ujifunze na kuondoka na mambo ya kwenda kufanyia kazi ili uweze kupiga hatua zaidi kwenye maisha yako.

Kocha.