May 23 • 3HR 6M

Ongea Na Kocha; Sell Like Crazy, Basil Danghalo.

 
1.0×
0:00
-3:06:28
Open in playerListen on);
Karibu kwenye vipindi vya sauti vya Ongea Na Kocha ambapo Kocha Dr Makirita Amani atakuwa anakushirikisha maarifa mbalimbali ya mafanikio pamoja na kujibu maswali na changamoto unazokutana nazo kwenye safari yako ya mafanikio.
Episode details
Comments

Habari Mwanamafanikio?

Karibu kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA ambapo kuna mambo mawili makubwa.

Jambo la kwanza ni mjadala wa pamoja wa kitabu cha SELL LIKE CRAZY. Hiki ni kitabu kilichoandikwa na Sabry Subi ambacho kinatupa maarifa ya kuweza kujenga mfumo wa masoko na mauzo ambao unatuwezesha kuleta wateja wengi kwenye biashara na kufanya mauzo makubwa kuliko tulivyozoea. Haya ni maarifa muhimu sana kwa ukuaji wa biashara zetu. Kwenye mjadala huu wa kitabu, wanamafanikio mbalimbali wameshirikisha yale waliyojifunza kwenye kitabu na uzoefu wao katika kufanyia kazi mambo hayo. Sikiliza kipindi kujifunza zaidi.

Jambo la pili ni mahojiano na mwanamafanikio mwenzetu Basil Danghalo ambaye anatushirikisha sehemu ya safari yake ya mafanikio. Anatueleza jinsi alivyoanza biashara kwa kuuza vocha na mpaka kuwa na duka moja na hatimaye maduka manne. Yote hayo ameweza kuyafanya akiwa mazingira ya kijijini kabisa huku akiwa bado ni mwajiriwa. Kupitia Basil tunajifunza mengi kuhusu safari ya mafanikio, hasa kupambania ndoto yako bila kujali wengine wanakuchukuliaje. Sikiliza kipindi kujifunza mengi zaidi kutoka kwa mwenzetu.

Karibu sana usikilize kipindi hiki uweze kujifunza na kwenda kuchukua hatua ili maisha yako yawe bora zaidi na uweze kuzifikia ndoto zako kubwa.

Kocha.