Apr 11 • 3HR 5M

Ongea Na Kocha; Kuongeza Kiwango Cha Faida, Mwongozo Wa Kufika Kwenye Ubilionea.

 
1.0×
0:00
-3:04:55
Open in playerListen on);
Karibu kwenye vipindi vya sauti vya Ongea Na Kocha ambapo Kocha Dr Makirita Amani atakuwa anakushirikisha maarifa mbalimbali ya mafanikio pamoja na kujibu maswali na changamoto unazokutana nazo kwenye safari yako ya mafanikio.
Episode details
Comments

Habari mwanamafanikio?

Karibu kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA ambacho kina mambo mawili makubwa.

Jambo la kwanza ni mjadala wa sehemu ya mwisho ya kitabu cha INSTANT CASHFLOW inayohusu kuongeza kiwango cha faida. Wanamafanikio wameshirikisha njia tano walizochagua kufanyia kazi kwenye biashara zao ili kuweza kuongeza kiwango cha faida. Ni njia nzuri na zinazowezekana kwa kila aina ya biashara.

Jambo la pili ni MWONGOZO WA KUFIKIA UBILIONEA. Nimeshirikisha mwongozo kamili tunaokwenda kufanyia kazi kwenye huu muongo (2020 – 2030) ili kila mmoja wetu aweze kufikia ubilionea na uhuru wa kifedha. Mkakati una hatua za kupiga kwenye kila mwaka wa mafanikio ambazo kila mmoja anapaswa kuzizingatia. Sikiliza kipindi kwa umakini mkubwa na pakua mwongozo uliopo hapa ili uweze kuchukua hatua sahihi.

Karibu usikilize kipindi na tuendelee kuweka juhudi kubwa ili kukamilisha jukumu kubwa ililo mbele yetu.

Kocha.