Mar 28 • 3HR 2M

ONGEA NA KOCHA; HELL YEAH, BOSCO MLOMO.

2
 
1.0×
0:00
-3:02:17
Open in playerListen on);
Karibu kwenye vipindi vya sauti vya Ongea Na Kocha ambapo Kocha Dr Makirita Amani atakuwa anakushirikisha maarifa mbalimbali ya mafanikio pamoja na kujibu maswali na changamoto unazokutana nazo kwenye safari yako ya mafanikio.
Episode details
Comments

Habari Mwanamafanikio?

Karibu kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA ambapo kuna mambo matatu makubwa.

Jambo la kwanza ni uchambuzi wa kitabu cha HELL YEAH OR NO kilichoandikwa na Derek Sivers. Kwenye kitabu hiki mwandishi ametushirikisha falsafa yake fupi ya kuchagua nini afanye. Anatuambia kama kitu hukipi NDIYO kubwa basi unapaswa kukipa HAPANA. Ni kitabu kifupi, chenye mambo ya kawaida ila yenye nguvu kubwa sana kwenye safari yetu ya mafanikio.

Jambo la pili ni mahojiano na mwanamafanikio mwenzetu Bosco Mlomo ambaye anatushirikisha safari yake ya kibiashara. Bosco anatushirikisha alivyoanza kama msaidizi kwenye duka la vifaa vya bomba akilipwa mshahara wa tsh elfu 60 kwa mwezi. Baadaye akapata fursa ya kuwanunulia watu bidhaa kariakoo na kuwatumia mikoani. Na hapo ndipo alipoona fursa ya yeye kuanza biashara. Ametushirikisha hatua kubwa alizoweza kupiga na changamoto ambazo amekuwa anakabiliana nazo. Kuna mengi ya kujifunza kutoka kwenye safari ya mwanamafanikio mwenzetu.

Jambo la tatu ni mjadala wa pamoja wa wanamafanikio wote ambao wameshirikisha yale waliyojifunza kutoka kwenye kitabu pamoja na kutoa ushauri kwa mwanamafanikio mwenzetu Bosco. Ushauri mzuri sana umetolewa kwake wa jinsi ya kuweza kukua zaidi na kuyafikia malengo yake. Kuna mengi mazuri ya kujifunza kutoka kwa wengine.

Tenga muda na usikilize kwa makini kipindi hiki, utoke na mambo ya kwenda kufanyia kazi ili kuwa imara kwenye safari ya mafanikio.

Karibu sana ujifunze na kuwa bora ili ufanikiwe zaidi.

Kocha.