Apr 25 • 3HR 8M

Ongea Na Kocha; How To Live On 24 Hours A Day Na Mwongozo Wa Kufanya Tathmini Ya Robo Mwaka.

 
1.0×
0:00
-3:08:23
Open in playerListen on);
Karibu kwenye vipindi vya sauti vya Ongea Na Kocha ambapo Kocha Dr Makirita Amani atakuwa anakushirikisha maarifa mbalimbali ya mafanikio pamoja na kujibu maswali na changamoto unazokutana nazo kwenye safari yako ya mafanikio.
Episode details
Comments

Habari Mwanamafanikio?

Karibu kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA ambacho kina mambo mawili makubwa.

Jambo la kwanza ni mjadala wa kitabu cha HOW TO LIVE ON 24 HOURS A DAY kilichoandikwa na Arnold Bennett. Kitabu hiki kifupi ambacho kimeandikwa zaidi ya miaka 100 iliyopita kina mengi ya kutufundisha kuhusu matumizi sahihi ya muda na jinsi ya kuishi vyema. Kwenye kipindi tumekuwa na mjadala wa kitabu ambapo wanamafanikio wameshirikisha yale waliyojifunza kwenye kitabu hicho.

Jambo la pili ni mwongozo wa kufanya tathmini ya robo mwaka. Tunamaliza robo mwaka ya pili kwenye mwaka wa mafanikio 2021/2022. Ni wakati wa kujifanyia tathmini ili kuweza kuona biashara zetu zimekwendaje kwa kipindi cha miezi mitatu. Kwenye kipindi hiki nimetoa ufafanuzi wa namna bora ya kujifanyia tathmini hiyo na umuhimu wa kila kipengele.

Karibu usikilize kipindi hiki ili uweze kujifunza na kuondoka na ya kwenda kufanyia kazi.

Kocha.