Google Ya Mafanikio
Ongea Na Kocha.
ONGEA NA KOCHA; Tathmini Ya Robo Mwaka, Kigawe Kikuu Cha Mafanikio, Instant Cashflow.
0:00
-3:05:08

ONGEA NA KOCHA; Tathmini Ya Robo Mwaka, Kigawe Kikuu Cha Mafanikio, Instant Cashflow.

Karibu kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA ambacho kina mambo yafuatayo.

Moja ni mrejesho wa tathmini za robo mwaka ya kwanza kwenye mwaka wa mafanikio 2021/2022. Nimeshirikisha yale muhimu kutoka kwenye tathmini hizo na namna ya kujiandaa vyema kwa tathmini ijayo.

Mbili ni andiko la KIGAWE KIKUU CHA MAFANIKIO (THE COMMON DENOMINATOR OF SUCCESS) ambalo linaelezea siri kuu ya mafanikio ambayo wote waliofanikiwa wameijua na kuifanyia kazi. Siri hiyo ni watu waliofanikiwa wamejijengea tabia ya kufanya vitu ambavyo walioshindwa hawapendi kuvifanya. Utajifunza kwa kina kutoka kwenye andiko hilo.

Tatu ni uchambuzi wa kitabu cha INSTANT CASHFLOW ambapo tunapata sehemu ya kwanza mpaka ya tatu ya kitabu. Kwenye uchambuzi huu tunajifunza kuhusu kubadili mtazamo wetu kuhusu biashara, kuwa bora kwenye masoko na injini kuu ya biashara. Ni maarifa ya msingi kabisa tunayopaswa kuwa nayo katika kujenga biashara zinazojiendesha bila kututegemea.

Nne ni mjadala wa pamoja wa wanamafanikio wote ambapo kuna mengi ya kujifunza. Pascal Kasanda anatushirikisha uzoefu wake kwenye masoko ya ana kwa ana na kutumia matangazo ya redio. William Loma anatushirikisha kisa chake chenye funzo kubwa cha kuuza samaki walioharibika. Hayo na mengine mengi kwenye mjadala yana makubwa ya kujifunza.

Karibu usikilize kipindi hiki, ujifunze kwa kina na kwenda kuchukua hatua ili maisha yako yazidi kuwa bora na ufikie ndoto zako kubwa.

Kocha.

0 Comments
Google Ya Mafanikio
Ongea Na Kocha.
Karibu kwenye vipindi vya sauti vya Ongea Na Kocha ambapo Kocha Dr Makirita Amani atakuwa anakushirikisha maarifa mbalimbali ya mafanikio pamoja na kujibu maswali na changamoto unazokutana nazo kwenye safari yako ya mafanikio.