"If you care too much about being praised, in the end you will not accomplish anything serious. People have differ ent values. You may say, “I want good people to value me,” but you know you will respect only those who praise your actions." - Leo Tolstoy
Kama unachotaka ni wengine wakusifie na kukubaliana na wewe kwa kila unachofanya, hutaweza kufanya mambo makubwa kwenye maisha yako.
Hiyo ni kwa sababu watu watakusifia pale unapofanya mambo wanayoyaelewa, na mambo wanayoyaelewa ni ya kawaida sana.
Sasa unajua kabisa kwamba kwa kufanya mambo ya kawaida, unapata matokeo ya kawaida na hivyo huwezi kupiga hatua kubwa.
Ili kupiga hatua kubwa na kufanikiwa zaidi, lazima uwe tayari kufanya mambo mapya na ya tofauti, ambayo hatajazoeleka na wengine.
Utakapoanza kufanya mambo hayo, watu hawatakuelewa, watakupinga, kukukosoa na kukukatisha tamaa.
Lazima uwe tayari kupokea hayo na kusonga mbele kama kweli unataka kufanikiwa.
Lakini kama unachotaka ni kusifiwa, utaishia kuwa kawaida.
Asubuhi ya leo tafakari kila unachofanya sasa kwenye kazi, biashara na maisha kwa ujumla.
Je wengi wanakubaliana na wewe na kukusifia au hawakuelewi.
Kama wanakuelewa sana, jua unachofanya siyo kikubwa na hakitakupa matokeo ya tofauti, utaishia tu kuwa kama wao.
Lakini kama hawakuelewi, wanatishwa na yale unayofanya kwa kuwa wanaona ni makubwa sana na yapo nje ya uwezo wako, basi upo kwenye njia sahihi ya kufika kwenye mafanikio makubwa.
Lengo lako kuu kwenye maisha ni kufika kule unakotaka kufika na siyo kusifiwa na kukubalika na wengine.
Hivyo weka umakini kwenye lengo hilo na puuza kutaka sifa za wengine.
Uzuri ni kwamba, utakapoyapata mafanikio makubwa, wale waliokuwa wanakupinga na kukukatisha tamaa, watakuwa ndiyo wa kwanza kukusaidia.
Weka mkazo kule unakotaka kufika na acha wengine wakuchukulie wanavyotaka wao.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu mafanikio ya asilimia 100, soma hapa; www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/11/02/2133
Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.
Asante sana kwa hii tafakari Kocha
Njia pekee ya kufanya mambo makubwa ni kuvuka kikwazo cha kufanya vitu ili usifiwe.