Google Ya Mafanikio
Ongea Na Kocha.
Johnbosco Boniphace; Safari ya Kibiashara.
0:00
-2:18:54

Johnbosco Boniphace; Safari ya Kibiashara.

Kuweza kukuzanya mtaji, kuanzisha na kukuza biashars.

Habari wanamafanikio?

Karibuni kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA ambapo mwanamafanikio mwenzetu Johnbosco Boniphace anatushirikisha safari yake ya biashara.

Kwenye kipindi hiki utajifunza yafuatayo;

  1. Jinsi alivyoweza kukusanya mtaji kupitia fedha ya kujikimu chuoni

  2. Jinsi alivyoweza kutumia changamoto kuona fursa ya kuanzisha biashara.

  3. Jinsi alivyokuwa king'ang'anizi mpaka kupata eneo zuri la kufanyia biashara.

  4. Nidhamu yake ya hali ya juu katika kuendesha biashara yake.

  5. Upinzani kutoka kwa wengine kutokana na mafanikio anayoanza kupata.

  6. Kuzushiwa imani za kishirikina kutokana na hatua za tofauti anazopiga.

  7. Msukumo wa jamii kuhusu kupata ajira na jinsi ya alivyoweza kuvuka hilo.

  8. Malengo makubwa aliyonayo kwenye biashara.

  9. Ratiba yake ya siku katika kuendesha biashara yake kwa ufanisi mkubwa.

  10. Ushauri aliopata kutoka kwa wengine.

Karibu usikilize kipindi hiki, kina mengi ya kujifunza ambayo yatakusaidia kupiga hatua zaidi kimafanikio.

Kocha.

0 Comments